9.3 C
New York

Adamu, kaka yake jela kwa wizi msikitini

Published:

ABUJA, Nigeria

MAHAKAMA ya Wilaya ya Wuse mjini Abuja imewahukumu ndugu wawili kifungo cha miezi minne gerezani kila mmoja baada ya kukutwa na hatia katika mashitaka ya wizi wa simu msikitini.

Adamu na Rabiu Ibrahim, ambao ni ndugu wamehukumiwa kifungo hicho, ingawa wanaweza kukiepuka endapo watalipa faini ya Naira 30,000 kila mmoja.

Kabla ya hukumu, Mahakama ilielezwa kuwa mlalamikaji, Yusuf Aliyu, alifungua kesi hiyo Januari 2, 2026.

Kwa mujibu wa kile kilichoelezwa mahakamani, Adamu na kaka yake, Rabiu, waliingia katika Msikiti wa Annur ulioko mjini Maitama, kama waumini wengine tu.

Lakini, wakati Yusuf akiendelea na swala, ndugu hao walishirikiana kumchomolea mfukoni simu yake ya kisasa aina ya Galaxy Fold 4.

Baada ya kukamatwa, wawili hao walikiri kuwa walitaka kwenda kuiuza, maelezo ambayo pia waliyatoa mahakamani.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img