8.4 C
New York

Mambo 10 usiyoyajua kuhusu kocha mpya Chelsea

Published:

LONDON, Uingereza

UONGOZI wa Chelsea umemtangaza kocha mpya atakayechukua nafasi ya Enzo Maresca. Anaitwa Liam Rosenior.

Je, ni yapi usiyoyajua kuhusu kocha huyo mwenye umri wa miaka 41? Makala haya yanachambua mambo 10.

Mosi, Rosenior ni raia wa Ufaransa na anatua Stamford Bridge akitokea Strasbourg ya Ligi Kuu ya Ufaransa.

Pili, Rosenior aliajiriwa na klabu hiyo Julai, 2024, na kuiwezesha kumaliza msimu ikiwa nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligue 1.

Tatu, Rosenior aliwahi kucheza soka, ambapo alizitumikia U-20 na U-21 za England akiwa beki wa pembeni.

Nne, Rosenior alistaafu rasmi kucheza soka mwaka 2018, wakati huo akiwa mchezaji wa Brighton.

Tano, alianza kazi ya ukocha mwaka 2022 akiwa na Derby County ya Ligi Daraja la Kwanza England (Championship).

Sita, alifukuzwa kazi mwaka 2024 akiwa kocha wa Hull City ya Championship. Ndipo alipoibukia Strasbourg.

Saba, Rosenior ni kocha anayependa uchezaji wa kumiliki mpira. Ni muumini wa mifumo ya 4-2-3-1 na 3-4-3.

Nane, ni kocha anayependa makinda. Ameifanya Strasbourg kuwa moja ya klabu zinazofanya vizuri katika soka la vijana.

Tisa, Rosenior aliwahi kumvaa Rais wa Marekani, Donald Trump. Alimkosoa kwa kauli zake za ubaguzi wa rangi.

Kumi, Rosenior amekiri kuwa kuinoa Chelsea ni moja ya ndoto zake za muda mrefu tangu akifanya kazi Championship.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img