MANCHESTER, Uingereza
HATIMAYE Manchester United wamemfuta kazi Ruben Amorim. Mreno huyo ameondoka akiwa amehudumu kwenye benchi la ufundi kwa miezi 14 pekee tangu alipoajiriwa akitokea Sporting Lisbon ya Ureno.
Amorim aliyeajiriwa kuchukua mikoba ya Erik ten Hag, ametimuliwa akiwa ameshinda asilimia 38 tu ya mechi alizoiongoza Manchester United. Ameshinda 24 kati ya 63.
Kwa upande mwingine, kuondoka kwake ni mwendelezo wa mateso wanayopitia makocha walioajiriwa na klabu hiyo tangu Alex Ferguson alipoondoka mwaka 2013.

Ferguson aliondoka Manchester United akiwa na mataji 26 lakini kila kocha aliyeajiriwa baada yake ameishia kufanya vibaya na hatimaye kufungashiwa virago.
Tangu alipotimka Old Trafford, Manchester United imekuwa chini ya makocha 10, ambao David Moyes, Louis van Gaal, Jose Mourinho, Ole Gunnar Solksjaer, Ten Hag, Amorim, Ryan Giggs, Michael Carrick, Rangnick na Ruud van Nistelrooy.
Hata hivyo, hakuna aliyefikia mafanikio ya Ferguson, achilia mbali kuifanya Manchester United irejeshe ubora wake uwanjani.
Kati ya hao 10, kocha pekee anayeweza kuonekana alikuwa na mafanikio ni Mourinho, ambaye alifukuzwa akiwa ameshinda asilimia 58.3 ya mechi alizoiongoza timu hiyo.
Pia, walau Mreno huyo aliiwezesha Manchester United kutwaa mataji matatu (Kombe la Ligi, Ligi ya Europa na Ngao ya Jamii) msimu wa 2016-17.
Ten Hag aliishia kutwaa mataji mawili, huku Van Gaal akibeba FA na Moyes akiambulia Ngao ya Jamii akiwa Old Trafford.