3.9 C
New York

HaloPesa yahitimisha kampeni ya “Tamba na Bonasi”, yawakabidhi zawadi

Published:

Na Imani Nathaniel, Gazetini

HaloPesa imehitimisha rasmi kampeni yake ya ‘Tamba na Bonasi’ baada ya kuwazawadia wateja wake zawadi mbalimbali zikiwemo bonasi na fedha taslimu hadi Sh 2,000,000, zilizokuwa zikitolewa kwa kipindi chote.

Katika kilele cha kampeni hiyo, ushindi mkubwa wa hundi ya sh 2,000,000 ulikabidhiwa kwa mshindi kutoka Zanzibar.

Kupitia kampeni hiyo, wateja wa HaloPesa walipata nafasi ya kushinda zawadi kila walipofanya miamala ya kawaida ikiwemo kutuma na kutoa pesa, kulipa bili pamoja na kulipia bidhaa.

Meneja Masoko wa HaloPesa, Aidat Lwiza, ameeleza kuwa kampeni hiyo ilikuwa sehemu ya maadhimisho ya miaka tisa ya HaloPesa na miaka 10 ya Halotel, ikiwa na lengo la kuhamasisha matumizi ya huduma za kifedha kidijitali nchini.

“Katika kipindi cha miaka tisa ya HaloPesa, tumefanikiwa kuwazawadia maelfu ya wateja wetu kupitia kampeni hii, kwa kuwapatia bonasi na fedha taslimu hadi shilingi Milioni mbili. Hii ni njia yetu ya kuwashukuru kwa kuendelea kutumia na kuamini huduma zetu,” amesema Aidat.

Aliongeza kuwa wataendelea kuboresha huduma zake kwa kutoa makato nafuu, ofa na promosheni mbalimbali zitakazorahisisha zaidi miamala ya kifedha na kuongeza thamani kwa wateja wake.

Aidha amewahakikishia wateja wao kuendelea kuwapatia huduma bora zaidi mwaka 2026 kwa kuimarisha mifumo ya kidijitali na kuboresha uzoefu wa wateja.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img