5.7 C
New York

Avunja rekodi ya kukumbatia mti kwa siku tatu

Published:

NAIROBI, Kenya

MWANAHARAKATI wa mazingira nchini Kenya, Truphena Muthoni, amevunja rekodi yake ya kukumbatia mti, safari hii akitumia siku tatu (saa 72) mfululizo.

Muthoni amefanya hivyo ikiwa ni kampeni yake ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira, ikiwa ni pamoja na kupinga ukataji wa miti.

Kwa kufanya hivyo, mwanaharakati huyo amevunja rekodi yake ya awali, ambapo alikumbatia mti kwa siku mbili mfululizo.

Safari hii, Muthoni alichagua kukumbatia mti uliopo jirani na jengo la Serikali mjini Nyeri, ambapo pia mashabiki wake walimzunguka wakimtazama.

Wakati fulani, alikaribia kuangukia usingizini lakini mashabiki wake waliendelea kumtia moyo, pia wakichangishana fedha za kuwaita watafiti wa Guinness World Records ili aingie kwenye rekodi za dunia.

Hatua hiyo imeungwa mkono duniani kote, wengine wakiyataja kuwa ni ‘maandamano ya amani’ yanayopaswa kuigwa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img