33.3 C
New York

Bangi yamzimisha mbwa, azinduka siku ya pili

Published:

LONDON, Uingereza

TIMU ya waokoaji wa Mlima Ben Nevis imelazimika kumuokoa mbwa aliyepoteza fahamu baada ya kutumia kilevi aina ya bangi.

Tukio hilo lilitokea wikiendi iliyopita, Julai 12, 2026, na aliyesimulia mkasa huo ni mmiliki wake, Christina Bluhme.

Siku hiyo, alikuwa naye kwenye safari ya kupanda mlima lakini ghafla mbwa huyo alizidiwa wakiwa nusu ya umbali wa futi 4,413 kufikia kilele cha Mlima huo.

Akizungumzia tukio hilo na kumtaja mbwa huyo kwa jina la Tokyo, Bluhme amesema: “Ghafla alipoteza nguvu ya kutembea, akapoteza fahamu.”

Bluhne ameeleza kuwa hali hiyo ilimfanya apige simu kwa timu ya uokoaji, ambayo ilifika na kumsaidia kumkimbiza hospitali ya wanyama akiwa hajitambui.

“Nisingeweza kumuokoa kutoka kule mlimani,” amesema Bluhme na kuongeza kuwa mbwa huyo alizinduka siku iliyofuata.

Related articles

Recent articles