27.2 C
New York

Sheikh Hamad wa Qatar afariki

Published:

DOHA, Qatar

KIONGOZI wa zamani wa Taifa la Qatar, Sheikh Hamad bin ⁠Khalifa Al Thani, ‌amefariki leo Julai 12, 2026, akiwa na umri wa miaka 74.

Sheikh Hamad ambaye aliiongoza Qatar kuanzia mwaka 1995 hadi 2013, atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika ujenzi wa uchumi wa mafuta nchini humo.

Pia, chini ya uongozi wake, Qatar iliweza kuwa Taifa linaloongoza kwa usafirishaji wa gesi asilia duniani.

Kutokana na heshima yake, Serikali ya Qatar imetangaza siku nne za maombolezo ya Kitaifa kuanzia kesho Julai 13, 2026.

Wakati wa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2022 zilizofanyika Qatar, Sheikh Hamad alishangiliwa vilivyo na mashabiki alipohudhuria mechi ya ufunguzi.

Moja ya alama nyingine kubwa ya utawala wake ni kuanzishwa kwa kituo cha televisheni cha Al Jazeera News mwaka 1996, ambacho kwa sasa ni moja ya vyombo vya habari vikubwa duniani.

Related articles

Recent articles