24.2 C
New York

Marekani yaitumia ujumbe mzito Iran

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

SERIKALI ya Marekani imeitaka Iran kuacha mara moja kuendeleza udhibiti wake katika Mlango-Bahari wa Hormuz.

Katika agizo hilo, Marekani imezitaka mamlaka za Iran kutangaza hadharani kuwa njia hiyo iko wazi kwa meli zote za mafuta na gesi.

Wikiendi hii, pande mbili za usuluhishi kutoka Marekani na Iran zilikutana na kufanya mazungumzo nchini Oman.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya Marekani, wawakilishi wa Iran walikiri kuwa lilikuwa ni kosa kubwa kuzishambulia meli zilizopita Hormuz.

Vyanzo hivyo vya habari vilieleza kuwa wawakilishi wa Iran walidai kwamba mashambulizi hayo yanatekelezwa na vikundi vya kigaidi.

Kwa upande mwingine, Rais Donald Trump amesema mazungumzo ya kusaka suluhu kati ya Marekani na Iran yanaendelea.

Related articles

Recent articles