NASSAU, Bahamas
AJALI ya ndege ndogo nchini Bahamas imesababisha vifo vya abiria tisa, pamoja na rubani wao, mamlaka za nchi hiyo zimeeleza.
Ndege hiyo ilikuwa ikifanya safari fupi kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Lynden Pindling jirani na Mji wa Nassau.
Kwa mujibu wa taarifa, iliangukia porini ikiwa umbali mfupi kufika katika Uwanja wa Ndege wa San Andros.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Bahamas, Philip Davis, amesema awali alipatikana abiria aliyekuwa hai lakini alifariki baadaye kutokana na majeraha.
Hata hivyo, bado Mamlaka za Usafiri wa Anga za Bahamas hazijaanika majina, umri na taarifa zingine binafsi za waliofariki katika ajali hiyo.


