29.8 C
New York

WHO yaonya kuhusu kasi ya saratani

Published:

NEW YORK, Marekani

SARATANI ni ugonjwa unaosababisha vifo 26,000 kila mwaka lakini idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka mara mbili ifikapo mwaka 2050.

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolea hivi karibuni na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO).

Kwa sasa, ripoti hiyo inaonesha kuwa kila mwaka kuna wagonjwa wapya milioni 20.6 na vifo milioni 10.

Kwamba saratani ni ugonjwa wa pili kwa kusababisha vifo vingi duniani, ikitanguliwa na magonjwa ya moyo.

Hivyo, WHO inaonya kuwa idadi hiyo itaongezeka mara mbili mwaka 2050 endapo jitihada za haraka hazitochukuliwa.

Ripoti ya Hali ya Saratani Duniani inaonesha kuwa ni asilimia 42 tu ya wanawake wanaokutwa na saratani ya matiti katika nchi masikini huweza kuishi ndani ya miaka mitano.

WHO inaeleza wasiwasi wake zaidi, ikionesha kuwa katika nchi nyingi, bado serikali hazibebi gharama za saratani ili kuwasaidia wananchi.

“Saratani ni ugonjwa unaomgusa kila mmoja wetu. Haijalishi umezaliwa wapi au una kipato kiasi gani,” amesema Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus.

Katika utafiti wake wa mwaka 2024, Bara la Asia lilionekana kuwa na idadi kubwa zaidi (50.7%) ya wagonjwa wa saratani duniani. Pia, iliongoza kwa vifo vingi (56%).

Kwa upande mwingine, saratani ya mapafu ndiyo inayotajwa na tafiti nyingi za WHO na taasisi zingine za afya kuongoza kwa idadi kubwa ya vifo duniani.

Hata hivyo, asilimia kubwa ya magonjwa ya saratani, ikiwamo ya mapafu, husababishwa na mitindo ya maisha, ikiwamo uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe na kutokufanya mazoezi.

Kwamba wakati huu matumizi ya tumbaku yakitajwa kupungua kwa asilimia 27, ugonjwa wa saratani ya mapafu nao umeripotiwa kupungua.

Related articles

Recent articles