LAGOS, Nigeria
POLISI nchini Nigeria wanamshikilia Dj maarufu, Chicken, akitajwa kumtishia maisha mtoto wa Rais Bola Tinubu, Seyi.
Kabla ya kukamatwa kwake, Dj Chicken alitumia siku mbili mitandaoni kumchafua Rais Tinubu.
Katika maelezo yake, Dj huyo alisema Rais Tinubu hana nafasi ya kupata ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2027.
Chicken alienda mbali zaidi na kusema atamuua Seyi endapo baba yake atashinda Uchaguzi huo.
Siku mbili baada ya kutoa kauli hizo, ziliibuka ripoti mbalimbali zikidai kuwa Dj huyo amekamatwa.


