BEIRUT, Lebanon
WAZIRI wa Mambo ya Nje ya Syria, Asaad al-Shaibani, yuko nchini Lebanon, ambapo amesema wako tayari kukaa mwezani na wapiganaji wa Kundi la Hezbollah.
Hezbollah inayoungwa mkono na Iran, ni moja ya vikundi vinavyohusishwa na ugaidi ndani ya Lebanon na Ukanda wa Mashariki ya Kati kwa ujumla.
Akiwa Lebanon, al-Shaibani amekutana na Rais Joseph Aoun, Waziri Mkuu, Nawaf Salam, na Spika wa Bunge, Nabih Berri, ambaye ni mshirika wa Hezbollah.
Kwa miaka mingi, Serikali ya sasa ya Syria imekuwa na uhusiano mbaya unaohusisha vita na wapiganaji wa Hezbollah.
Ugomvi huo ulitokana na Hezbollah kuunga mkono utawala wa Syria uliopita chini ya Rais Bashar al-Assad.
Awali, mamlaka za Syria ziliweka wazi kuwa nchi hiyo haitoingilia vita vinavyoendelea nchini Lebanon kati ya Hezbollah na wanajeshi wa Israel.


