37.6 C
New York

Hii ndiyo Mexico inayosumbua Kombe la Dunia

Published:

MEXICO CITY, Mexico

LICHA ya kuchukuliwa poa hata kabla ya michuano ya Kombe la Dunia kuanza Juni 11, 2026, Mexico ni moja ya timu zilizofanya balaa msimu huu.

Wenyeji hao wa michuano kwa kushirikiana na Marekani na Canada, wako hatua ya 16 Bora baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ecuador.

Bao la kuongoza likifungwa na Julian Quinones, kisha nyota huyo akatoa ‘asisti’ kwa Raul Jimenez aliyefunga la pili.

Hiyo ilikuwa mechi ya nne katika fainali hizo na sasa Mexico imefikisha mabao nane ya kufunga, sawa na mawili kila dakika 90, huku ikiwa haijaruhusu nyavu zake kutikiswa.

Katika hatua ya makundi, ilivuka ikiwa na pointi tisa baada ya kuzifunga Afrika Kusini, Jamhuri ya Czech na Japan, kabla ya kukutana na Ecuador hatua ya 32 Bora.

Baada ya kuitoa Ecuador, Mexico inaisubiri England katika hatua ya 16 Bora. Mechi ya kusaka tiketi ya kuingia robo fainali.

England ya kocha Thomas Tuchel imetoka kuing’oa DRC katika hatua ya 32 Bora kwa kuifunga mabao 2-1, mfungaji kwa upande wao akiwa ni nahodha Harry Kane.

Sasa, wataivaa Mexico na mechi hiyo itachezwa wikiendi hii, Juni 5, 2026, katika Uwanja wa Azteca.

Mexico haijafungwa katika mechi zote 10 za Kombe la ilizowahi kucheza hapo. Imeshinda nane na kupata sare mbili.

Pia, angalizo jingine kwa England ni kile kilichoikuta Ujerumani, ambayo licha ya kupewa nafasi kubwa, imeondoshwa na Paraguay katika michuano ya mwaka huu.

Related articles

Recent articles