24.8 C
New York

Yanayowakuta Wapalestina magereza ya Israel yanatisha

Published:

JERUSALEM, Israel

WANAHARAKATI wa haki za binadamu duniani wanataka kuona Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) ikiichunguza Israel juu ya uhalifu dhidi ya binadamu kwa raia wa Palestina.

Kwa mujibu wa wanaharakati, vikosi vya jeshi la Israel vimekuwa vikiwafanyia unyanyasaji wa kingono Wapalestina inaowateka kutoka Gaza.

Tangu Oktoba, 2023, wanaharakati wamekuwa wakilaani kinachofanywa na Israel dhidi ya raia wa Kipalestina inaowashikilia katika magereza.

Kwa mujibu wao, Israel imekuwa na vituo vya kuwashikilia na kuwatesa Wapalestina tangu mwaka 1967. Sde Teiman, ambayo awali ilikuwa kambi ya kijeshi ya Israel, kwa sasa ni moja ya vituo hivyo vya mateso.

Idadi ya raia wa Palestina walioingia katika magereza hayo tangu 2023 ni zaidi ya 750,000, kwa mujibu wa takwimu za wanaharakati.

Hata hivyo, kwa sasa magereza ya Israel yanatajwa kuwashikilia Wapalestina takribani 9,500, wakiwamo watoto zaidi ya 360.

Kati ya hao 95,00, zaidi ya 1,300 wameendelea kurundikwa magerezani pasi na kufunguliwa mashitaka.

Katika ripoti yake, Gazeti la Haaretz la Israel limewataja viongozi waandamizi wa jeshi la nchi hiyo kuwa wahusika wakubwa wa mateso dhidi ya Wapalestina walioko magerezani.

Miongoni mwa waliotajwa na chanzo hicho cha habari ni Mkuu wa Usalama wa Taifa, Itamar Ben-Gvir, na Kamishina Mkuu wa Polisi, Kobi Yaakobi.

Raia wa Palestina wanaoshikiliwa katika magereza ya Israel wameripotiwa kukumbana na kadhia mbalimbali zinazokinzana na haki za binadamu.

Baadhi ya matukio ya kikatili yanayoripotiwa zaidi ni kunyimwa matibabu, kuvuliwa nguo, kupigwa, kubakwa, kuingizwa vitu sehemu za siri, au hata kulazimishwa kufanya mapenzi na mbwa.

Related articles

Recent articles