LAGOS, Nigeria
MWIGIZAJI maarufu wa soko la filamu la Nigeria (Nollywood), Nancy Isime, amesema haoni kama anaweza kufurahia ndoa akiwa na mwanaume asiye na kipato kikubwa.
Nancy ametoa maoni hayo alipokuwa akizungumzia uhusiano uliopo kati ya fedha, mahusiano na ndoa.
Amesema si yeye tu, bali mwanamke yeyote hawezi kufurahia maisha akiwa na mwanaume masikini.
“Ndoa siyo chanzo cha kuondosha umasikini lakini siamini kama kuolewa na masikini kutakupa furaha,” amesema.
“Kodi inapokwisha, ada za watoto zinapodaiwa, chakula kinapokosekana, huwezi kufurahia maisha.”
Hata hivyo, bibiye huyo amedai kuwa hamaanishi hakuna mapenzi bila pesa. “Lakini kuna tofauti kati ya mapenzi na maisha mazuri,” amesisitiza.


