25.1 C
New York

Kamanda wa polisi Mkoa wa Tabora afariki dunia

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Richard Abwao, amefariki dunia leo Juni 20, 2026 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.

Kifo cha ofisa huyo kimethibitishwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime, ambaye amesema Abwao alikuwa akipatiwa matibabu hospitalini hapo kabla ya mauti kumkuta.

“Ni kweli aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Richard Abwao, amefariki dunia leo Juni 20, 2026 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa anapatiwa matibabu,” amesema Misime.

Amesema taarifa zaidi kuhusu taratibu nyingine zitakazofuata zitatolewa baadaye na Jeshi la Polisi.

Related articles

Recent articles