16.9 C
New York

Miezi mitatu baada ya kifo, Khamenei kuzikwa Julai

Published:

TEHRAN, Iran

MAMLAKA za Iran zimetangaza kuwa kiongozi wake Mkuu aliyeuawa Februari, 2026, Ali Khamenei, atazikwa mwezi ujao, Julai 9, mjini Mashhad.

Awali, Ali Khamenei alitarajiwa kuzikwa Machi, 2026 lakini ilishindikana kutokana na vita vinavyoendelea kati ya Iran na Marekani.

Khamenei (86), ambaye aliiongoza Iran tangu mwaka 1989, aliuawa Februari, 2026, baada ya makazi yake kushambuliwa na vikosi vya Marekani na Israel.

Aliingia madarakani wakati huo baada ya kifo cha Ayatollah Ruhollah Khomeini aliyeongoza mapinduzi ya Kiislam nchini humo.

Baada ya kuuawa kwa Khamenei, mtoto wake wa kiume, Mojtaba Khamenei, alichaguliwa kushika nafasi yake lakini amekuwa mafichoni kwa muda wote huo.

Related articles

Recent articles