LOS ANGELES, Marekani
TIMU ya soka ya Taifa ya Marekani imeanza na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Paraguay katika mechi ya Kundi D msimu huu wa fainali za Kombe la Dunia.
Wakati huo huo, bao la dakika ya saba walilopata Marekani ni la mapema zaidi kwa timu mwenyeji tangu Ujerumani ilipofunga mwaka 2006.
Mechi hiyo ya alfajiri ya leo Juni 13, 2026 imechezwa katika Uwanja wa SoFi, ikiwa pia ni mara ya kwanza kwa Marekani kufunga mabao manne ya mchezo mmoja wa Kombe la Dunia.
Msimu uliopita, wakati michuano hiyo ilipofanyika Qatar mwaka 2022, Marekani ilimaliza ikiwa na mabao matatu pekee.
Kituo kinachofuata
Marekani watarudi uwanjani Juni 19, 2026 kwa mchezo wa pili dhidi ya Australia kwenye Uwanja wa Seattle.
Siku hiyo pia, Paraguay watakuwa na kibarua cha kumenyana na Uturuki, mchezo utakaochezwa katika Uwanja wa San Francisco Bay Area.


