32.7 C
New York

Ndugu wanaocheza timu tofauti Kombe la Dunia 2026

Published:

MEXICO CITY, Mexico

FAINALI za Kombe la Dunia za mwaka huu (2026) zinaendelea katika mataifa matatu ya Marekani, Mexico na Canada.

Wakati huo huo, wapo wachezaji wanaotoka familia au ukoo mmoja lakini wanawakilisha mataifa tofauti kwenye michuano hiyo.

Miongoni mwao ni Desire na Guela Doue. Desire mwenye umri wa miaka 21, ni kiungo wa timu ya Taifa ya Ufaransa.

Katika ngazi ya klabu, nyota huyo anakipiga Ligue 1 akiwa na kikosi cha PSG kilichotwaa mara mbili mfululizo taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kaka yake, Guela, ni beki wa Ivory Coast na ana umri wa miaka 23. Nyota huyo anayecheza beki wa kulia, naye anacheza Ligue 1 akiwa na kikosi cha RC Strasbourg.

Wakati huo huo, kuna Inaki na Nico Williams. Inaki (31), ni mshambuliaji na yuko kwenye fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu akiwa na kikosi cha Ghana ‘Black Stars’.

Vilevile, katika ngazi ya klabu, Inaki ni nahodha wa Athletic Bilbao, akiipa timu hiyo ya La Liga mataji matatu; Copa del Rey (2023-24) na Supercopa de Espana (2015 na 2020).

Mdogo wake, Nico, ana umri wa miaka 23. Ni kiungo wa pembeni (winga) anayecheza timu ya Taifa ya Hispania na ni mchezaji wa klabu ya Bilbao anayoitumikia kaka yake.

Related articles

Recent articles