32.7 C
New York

Bafana Bafana waitangazia vita Czech

Published:

MEXICO CITY, Mexico

BAADA ya kufungwa mabao 2-0 na wenyeji Mexico, beki wa timu ya soka ya Taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’, Ime Okon, amesema wanahizitaji pointi tatu za mechi ijayo.

Jahazi la Bafana Bafana katika mchezo huo wa kwanza wa Kundi A lilizamishwa kwa mabao ya Julian Quinones na Raul Jimenez.

Kwa upande wake, Okon amesema ni bora wachezaji wenzake wakasahau kilichotokea na kujiandaa kisaikolojia kwa mechi ijayo dhidi ya Czech.

“Mechi ilikuwa ngumu, kuna wakati tuliwakamata. Tunajipanga kwa yajayo, tuko imara. Tunajua tumepoteza lakini tunaangalia mechi ijayo,” amesema.

Hata hivyo, dhidi ya Czech haitokuwa kazi rahisi kwa ‘Wasauzi’ kwani wenzao hao nao walipoteza mechi yao ya kwanza kwa kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Korea ya Kusini.

Related articles

Recent articles