34.1 C
New York

‘Special One’ atambulishwa Santiago Bernabeu

Published:

MADRID, Hispania

KLABU ya Real Madrid imemtambulisha rasmi Jose Mourinho kuwa kocha wao. Mreno huyo mwenye umri wa miaka 63 amesaini mkataba wa miaka mitatu kurudi Santiago Bernabeu.

Ripoti zinaeleza kuwa ‘Special One’ ataanza kazi rasmi Julai 13, 2026, siku ambayo Madrid itaanza kambi ya kujiandaa na msimu ujao (2026-27).

Mourinho amerudi Madrid ikiwa ni miaka zaidi ya 10 tangu alipoondoka. Klabu hiyo imelipa Pauni milioni 13 kuvunja mkataba wake na Benfica ya Ureno.

Ikumbukwe, ilikuwa ni ahadi ya Rais Florentino Perez kumrejesha kocha huyo endapo angeshinda katika Uchaguzi uliofanyika siku chache zilizopita.

Perez mwenye umri wa miaka 79, ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2009, ameshinda kiti cha urais kwa asilimia 65 ya kura, akimpiga bao mfanyabiashara mwenzake, Enrique Riquelme.

Related articles

Recent articles