34.1 C
New York

Rodriguez: Diaz apewe Ballon d’Or yake tu

Published:

MADRID, Hispania

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Real Madrid, James Rodriguez, amesema staa wa Bayern Munich winger, Luis Diaz, ndiye anayestahili tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka huu ya Ballon d’Or.

Rodriguez amedai kuwa nyota huyo, ambaye ni raia mwenzake wa Colombia, atastahili zaidi endapo mwaka huu ataifikisha timu hiyo hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia.

Wakati huo huo, amemtaja Diaz kuwa ni miongoni mwa wachezaji bora watano duniani kwa sasa. “Kwa upande wangu, ni miongoni mwa wale bora watano,” amesema Rodriguez.

Diaz amekuwa kwenye kiwango bora tangu alipotua Bayern akitokea Liverpool. Aliiwezesha kutwaa taji la Bundesliga msimu wa 2025-26 uliomalizika hivi karibuni.

Kutokana na kiwango chake kizuri, nyota huyo amekuwa akihusishwa na klabu zingine kubwa za Ulaya, zikiwamo PSG na Manchester City.

Related articles

Recent articles