TOKYO, Japan
KIUNGO wa timu ya Taifa ya Japan, Wataru Endo, ametangaza kustaafu soka hata kabla ya kucheza mechi yao ya kwanza msimu huu wa Kombe la Dunia dhidi ya Uholanzi (Juni 14, 2026).
Nyota huyo wa Liverpool mwenye umri wa miaka 33, amefikia uamuzi huo baada ya kupata majeraha ya enka yatakayomfanya akose mechi zote.
Endo alikosa msimu wote wa 2025-26 baada ya kufanyiwa upasuaji wa enka, kabla ya kujiunga na kikosi cha Japan akionekana ameshakuwa fiti.
Hivi karibuni, alicheza dakika 45 za mechi yao ya kujiandaa na Kombe la Dunia dhidi ya Iceland, ambapo walishinda bao 1-0.
Hata hivyo, taarifa za sasa zinaeleza kuwa alipata majeraha mengine kwenye eneo hilo la kifundo cha mguu, hivyo atakosa mechi zote za Kombe la Dunia.
Baada ya kuumia kwake, kitambaa cha unahodha amekabidhiwa beki wa Ajax ya Uholanzi, Ko Itakura, na nafasi yake kikosini imechukuliwa na mshambuliaji wa Borussia M’gladbach, Shuto Machino.


