34.1 C
New York

Mexico yaizima Afrika, yaitandika Bafana Bafana

Published:

MEXICO City, Mexico

TIMU ya soka ya Taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ imeanza na mguu mbaya fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu (2026) baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa wenyeji Mexico.

Katika mchezo huo wa ufunguzi, Mexico walipata bao la kwanza kupitia kwa Julian Quinones katika dakika ya 9, kabla ya Raul Jimenez kugongelea msumari mwingine dakika ya 67.

KADI NYEKUNDU TATU

Mechi hiyo imeshuhudia kadi nyekundu tatu, ambazo mbili zilikwenda kwa wachezaji wa Bafana Bafana, Themba Zwane na Yaya Sithole, na moja ikielekea kwa Cesar Montes wa Mexico.

Hiyo inakuwa mechi ya kwanza katika historia ya fainali za Kombe la Dunia kushuhudia kadi nyekundu tatu za moja kwa moja (bila njano) tangu mwaka 1998.

Lakini, inakuwa mechi pekee ya ufunguzi katika historia ya michuano hiyo kushuhudia nyota watatu wakiitwa na mwamuzi na kulimwa kadi nyekundu.

KITUO KINACHOFUATA

Baada ya mchezo huo wa kwanza, Mexico watatupa karata yao ya pili kwa kuikabili Korea ya Kusini katika mtanange utakaochezwa Juni 19, 2026.

Kwa upande wao, Bafana Bafana watakuwa na nafasi ya kujiuliza na kurekebisha makosa watakapokutana na Jamhuri ya Czech katika mechi ya Juni 18, 2026.

Related articles

Recent articles