25.9 C
New York

Watatu wakamatwa mauaji ya mwanamuziki

Published:

LONDON, Uingereza

POLISI nchini Uingereza wamewakamata watu watatu wanaohusishwa na tukio la kuuawa kwa staa wa muziki mwenye asili ya Nigeria, Mark Orabiyi.

Orabiyi aliyeuawa akiwa na miaka 35, alichomwa na kitu chenye ncha kali na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake hivi karibuni.

Taarifa ya polisi imeeleza kuwa walifika nyumbani kwake na kukuta akiwa kwenye bustani, wakati huo mwili ukiwa na majeraha mengi.

Aidha, polisi wamesema kati ya watu watatu waliokamatwa, wawili ni wanaume na mmoja ni mwanamke.

Hata hivyo, mmoja mwenye umri wa miaka 27 ameachiwa kwa dhamana, wakati wawili wenye miaka 24 na 25 wameachiwa baada ya kuhojiwa na kuonekana hawakuhusika.

Related articles

Recent articles