25.9 C
New York

Wananchi wa Iran walia vita kupaisha bei ya vyakula

Published:

TEHRAN, Iran

KUPANDA kwa gharama za maisha ni moja ya changamoto kubwa wanazopitia raia wa Iran kipindi hiki nchi yao ikiwa kwenye vita dhidi ya Marekani inayoshirikiana na Israel.

Kwa sasa, familia nyingi nchini Iran zinalalamikia kupanda kwa bei ya vyakula, hasa mchele na maziwa, hivyo wengi kushindwa kumudu.

Katika mahojiano yake na DW, mmoja ya raia amesema bei ya mchele imepanda kwa asilimia 9 ndani ya wiki mbili tu za hivi karibuni.

Wakati huo huo, bei za nyama ya kuku na maziwa nazo zimeripotiwa kupanda kwa asilimia 50, yaani mara mbili ya awali.

Tangu vilipoanza Februari 28, 2026, vita kati ya Iran na ushirika wa Marekani na Israel vimeonekana kukosa ufumbuzi, licha ya jitihada za hapa za pale za pande mbili hizo kukaa mezani.

Related articles

Recent articles