25.9 C
New York

Staa wa filamu afunguka mazito aliyofanyiwa na mkewe

Published:

LAGOS, Nigeria

MWIGIZAJI mkongwe wa Nigeria, Tioruju Mondusi, amefichua kuwa aliwahi kuambiwa na mkewe, kwamba kati ya watoto wao watano kwenye ndoa yao, wawili wana baba zao.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni, Mondusi aliulizwa na mwandishi wa habari juu ya siku aliyowahi kuumia zaidi kwenye maisha yake.

Anasema siku hiyo alitoka kazini lakini aliporudi nyumbani hakumkuta mkewe, ambaye wakati huo alikuwa na ujauzito wa mtoto wao wa tano.

Baadaye, mkewe (sasa maehemu) alirudi na kuanza kumtolea lugha chafu, alimwambia kuwa tayari ana mwanaume mwingine, hivyo ni bora waachane.

“Mtu pekee aliyewahi kuniumiza zaidi kwenye maisha ni mke wangu. Tukio hilo liliniliza. Kwa sasa ameshafariki. Mungu amsamehe,” anasema.

Related articles

Recent articles