LAGOS, Nigeria
MEJA Jenerali Mstaafu wa jeshi nchini Nigera, Rabe Abubakar, ametekwa na watu wasiojulikana akiwa na mkewe kwenye gari wakati wakiwa safarini katika Jimbo la Katsina.
Meja Jenerali alikuwa Msemaji wa jeshi kuanzia mwaka 2015 hadi 2017 alitekwa Mei 30,2026, kwa mujibu wa taarifa ya jeshi.
Kwa upande wake, Jenerali Michael Onoja amesema jitihada za kumkomboa Mstaafu huyo zinaendelea, sambamba na kuwatia nguvuni watekaji.
Tukio hilo ni mwendelezo wa hali mbaya ya usalama katika maeneo mengi nchini Nigeria, ambapo watekaji wamekuwa wakiwashikilia raia na kushinikiza kupewa fedha ili kuwaachia.
Desemba 25, 2025, Marekani ilitekeleza shambulizi la anga katika iliyotajwa kuwa ni kambi ya waasi ndani ya Jimbo la Sokoto.


