15 C
New York

Nje ya soka, hii hapa ‘pisi kali’ ya Mikel Arteta

Published:

LONDON, Uingereza

ACHANA na ndani ya uwanja, ambako tayari ameshaweka rekodi ya kuipa Arsenal taji la Ligi Kuu ya England (EPL) baada ya klabu hiyo kusubiri kwa miaka 22, akifanya hivyo ndani ya miaka saba tu tangu aajiriwe.

Nje ya uwanja, Mikel Arteta ni mume wa bibiye Lorena Bernal, ambaye ni mshindi wa zamani wa Shindano la urembo nchini Hispania na kuingia ‘Top 10’ ya Miss World.

Bernal, raia wa Hispania mwenye asili ya Argentina, ana umri wa miaka 45, akimzidi mmoja Arteta, na kwa sasa ni mama wa watoto watatu; Gabriel, Daniel na Oliver.

Alizaliwa Argentina, kabla ya kuhamia mjini San Sebastian, Hispania, akiwa mdogo. Ni Mji ambao pia ndiko walikozaliwa na kukulia Arteta na Xabi Alonso (kocha wa Chelsea).

Mlimbwende huyo, ambaye ni mzungumzaji mzuri wa lugha tatu – Kifaransa, Kihispania na Kiingereza – alianza kujihusisha na tasnia ya mitindo akiwa na umri wa miaka saba tu.

Akiwa na miaka 17, Bernal alitwaa taji la urembo la Hispania. Kwa ushindi huo, aliiwakilisha Hispania katika mashindano ya dunia na kuingia ‘Top 10’.

Mwaka 2002, alikutana na Arteta kwa mara ya kwanza katika ukumbi wa starehe wakati wa usiku. Ni wakati ambao Arteta alirudi likizo baada ya Ligi Kuu ya Scotland kumalizika akiwa na kikosi cha Rangers.

Walianzisha uhusiano wa kimapenzi, kabla ya wawili hao kufunga ndoa mwaka 2010. Mbali ya mitindo, Bernal aliwahi pia kuigiza, akitokea katika tamthilia ya ‘Chuck and CSI: Miami’.

Katika watoto wao watatu, wa kwanza mwenye umri wa miaka 16, Gabriel, anajaribu kufuata nyayo za baba yake. Anacheza nafasi ya winga katika kikosi cha U-18 ya Arsenal.

Related articles

Recent articles