12.9 C
New York

WHO: Unywaji wa pombe chanzo cha vifo milioni 2 kila mwaka

Published:

NEW YORK, Marekani

SHIRIKA la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) limeeleza katika ripoti yake ya hivi karibuni, kwamba unywaji wa pombe husababisha vifo milioni 2.6 kila mwaka.

WHO imeeleza hayo, huku utumiaji wa kilevi hicho ukiendelea kushika kasi katika jamii nyingi, ukihusianishwa na umataduni wa kisasa, starehe, au njia ya kupoteza mawazo.

“Matumizi ya pombe ni chanzo cha vifo milioni 2.6 duniani kila mwaka, pia ukisababisha changamoto za kiafya kwa mamilioni ya watu,” imeeleza ripoti hiyo ya WHO.

Katika hatua nyingine, Ripoti imefichua kuwa asilimia 4.7 ya magonjwa duniani hutokana na unywaji wa pombe, huku wanaume wakiwa waathirika zaidi.

“Kwa wanaume, asilimia 6.9 ya magonjwa hutokana na ulevi wa pombe. Kwa wanawake, ni asilimia 2.0,” imefafanua zaidi Ripoti hiyo.

Aidha, kwa vijana wa umri kati ya miaka 20 na 39, bila kujali jinsia zao, unywaji wa pombe huchangia vifo vya mapema kwa asilimia 13, kwa mujibu wa Shirika hilo.

Related articles

Recent articles