12.9 C
New York

Bao la Mpanzu laishusha Yanga kileleni

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini
BAO pekee la Elie Mpanzu katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji limeiwezesha Simba kushika usukani wa msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa tofauti ya pointi moja dhidi ya Yanga.
Katika mechi hiyo iliyochezwa leo Mei 24, 2026, kwenye Uwanja wa KMC, Mwenge jijini Dar es Salaam, Mpanzu alifunga kwa kumalizia mpira wa penalti ya Clatous Chama iliyookolewa na mlinda mlango wa Dodoma Jiji.
Usindi huo umewafanya Wekundu wa Msimbazi kufikisha pointi 58, wakati Yanga ikishuka hadi nafasi ya pili ikiwa na pointi 57.
Hata hivyo, Simba wamefikisha michezo 25, huku Yanga wakiwa na 24 na wakitarajiwa kushuka dimbani kesho Mei 25 kuikabili Namungo kwenye Uwanja wa KMC.
Wakati huo huo, matokeo ya leo ni mwendelezo wa ubabe wa Simba mbele ya Dodoma Jiji. Katika mechi sita za hivi karibuni, wameshinda tano na kutoa suluhu (0-0) moja.

Related articles

Recent articles