21.4 C
New York

Yanga, Azam zinatisha viwanja vya nyumbani

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini

MSIMU wa Ligi Kuu Bara unaelekea ukingoni, huku Yanga na Azam zikiwa ndizo timu pekee ambazo hadi sasa hazijafungwa katika mechi za nyumbani.

Yanga, mabingwa watetezi, ambao sasa wanaongoza Ligi wakiwa na pointi 54 dhidi ya 52 za Simba inayoshika nafasi ya pili, wamecheza mechi 11 za nyumbani msimu huu.

Katika michezo hizo, hakuna waliyofungwa, na badala yake wameshinda 10 na kupata sare moja, wakifunga mabao 37, wakiruhusu mawili, na kukusanya pointi 31.

Kwa upande wa Azam, wao msimu huu wamecheza mechi 11 pia, ambapo wameshinda saba na kutoa sare nne, wakifumania nyavu mara 24 na kuruhusu mabao matano.

Matajiri hao wa Chamazi, Temeke jijini Dar es Salaam, wametumia michezo hiyo 11 kukusanya pointi 25 kati ya 46 walizonazo kufikia hatua hii ya msimu wa 2025-26 wa Ligi Kuu Bara.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img