14 C
New York

Mbunge ataka shule jumuishi kila mkoa

Published:

Na Ramadhan Hassan, Gazetini

Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha kundi la watu wenye ulemavu, Nasria Nasri Ally, ameishauri Serikali kujenga shule jumuishi katika kila mkoa ili kurahisisha upatikanaji wa elimu kwa watoto wenye ulemavu.

Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Elimu bungeni jijini Dodoma Mei 8, 2026, Nasria alisema watoto wengi wenye ulemavu hulazimika kusafiri umbali mrefu kutafuta shule zinazotoa elimu maalumu, hali inayowaongezea changamoto za masomo na maisha.

Mbunge huyo pia ameshauri lugha ya alama ifundishwe kama somo rasmi kuanzia shule za msingi ili kuongeza ujumuishaji katika mfumo wa elimu nchini.

Aidha, aliitaka Wizara ya Elimu kushirikiana kwa karibu na wadau wa elimu maalumu pamoja na vyama vya watu wenye ulemavu wakati wa kuandaa mitaala, sera na miongozo ya elimu.

Nasria alisema watu wenye uziwi wanakabiliwa na mazingira magumu ya ujifunzaji yanayowalazimu baadhi yao kutumia muda mrefu zaidi kumaliza masomo.

Pia ameomba Serikali kuboresha miundombinu ya shule, kuongeza walimu wa elimu maalumu na kuhakikisha watoto wenye ulemavu wanajumuishwa katika mpango wa Bima ya Afya kwa Wote.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img