16.3 C
New York

Usiyoyajua kuhusu Siku ya Malaria Duniani

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

LEO Aprili 25, 2026 ni Siku ya Malaria Duniani na kaulimbiu ni “Lengo ni Kutokomeza Malaria: Sasa Tunaweza. Tunapaswa Kutokomeza.”

Kaulimbiu hiyo inabeba ujumbe kwamba ni jambo linalowezekana kutokomeza ugonjwa huo, lakini jitihada zaidi zinahitajika.

Siku ya Malaria Duniani iliasisiwa mwaka 2007 na Mkutano Mkuu wa Shirika la Afya la Kimataifa (WHO) kwa lengo la kuhamasisha uwekezaji zaidi katika kinga na tiba ya ugonjwa huo.

Jitihada zilizofanyika zimezaa matunda, ikiwamo takwimu kuonesha kuwa nchi 37 duniani ziliripoti visa vipya vya Malaria visivyozidi 1000 kwa mwaka 2024.

Kwa upande mwingine, kufikia mwaka 2025, nchi 47 duniani zilitangazwa kuondokana kabisa na ugonjwa wa Malaria.

Hata hivyo, bado kuna kazi kubwa ya kufanya katika maeneo mengi. Mwaka 2024, visa vipya vya Malaria vilifikia milioni 282 duniani kote, huku vifo vikiwa ni 610,000. Hiyo ni kwa mujibu wa Ripoti ya Malaria Duniani.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img