9.5 C
New York

Basi laingia mtoni, watu 24 wafariki

Published:

DHAKA, Bangladesh

WATU takribani 24 wamepoteza maisha baada ya basi walilokuwamo kupinduka na kuingia mtoni mjini Dhaka, Bangladesh.

Ajali hiyo imetokea leo Machi 26, 2026 wakati basi hilo likitoka Kusini-Magharibi kuelekea mjini Dhaka.

Basi hilo liliangukia katika Mto Padma wakati dereva akijaribu kulipitisha katika kivuko, umbali wa maili 10 kutoka Dhaka.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na polisi, basi hilo lililokuwa na watu 40 hadi 50 lilizama kina cha futi 30.

‌Inaelezwa kuwa asilimia kubwa ya abiria waliweza kujinasua, huku wengine wakipoteza maisha kwa kubanwa na gari.

Kati ya hao waliopoteza maisha, sita ni wanaume, 11 ni wanawake, na watano ni watoto.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img