HII ndiyo ‘psychology’ ya pesa ambayo watu wengi hawaielewi. Wengi wanafikiri umasikini unatokana na kukosa pesa.
Lakini ukweli ni kwamba mara nyingi hunasababishwa na mtazamo wa pesa (money mindset).
Unaweza kupata pesa nyingi lakini kama fikra zako hazijabadilika, pesa itaondoka haraka. Hizi ndizo sababu 6 kuu.
Mosi, ‘Lifestyle inflation’ (maisha kupanda kadiri pesa zinavyoongezeka. Watu wengi wakipata pesa zaidi huanza kubadilisha maisha haraka; kununua vitu vya gharama na kuongeza matumizi.
Mfano; simu mpya kila mwaka, gari kubwa kuliko uwezo au maisha ya kuonyesha watu.
Matokeo yake, kipato kinaongezeka lakini uhuru wa kifedha hauongezeki.
Pili, kutaka kuonekana tajiri badala ya kuwa tajiri. Kuna tofauti kubwa kati ya kuonekana tajiri na kuwa tajiri.
Watu wengi hununua vitu vya kuonyesha hadhi: nguo za bei kubwa, magari ya kifahari au sherehe kubwa.
Utakutwa wanaacha ‘investments’ (uwekezaji), ‘assets’ au kuweka mfumo wa kipato. Utajiri wa kweli mara nyingi haupigi kelele.
Tatu, hawajui kusimamia pesa (financial discipline). Kupata pesa ni ‘skill’ moja. Kusimamia pesa ni skill nyingine kabisa.
Watu wengi hawana bajeti, mpango wa uwekezaji na nidhamu ya matumizi. Ndiyo maana wanapata pesa nyingi lakini mwisho wa mwezi hawajui pesa imeenda wapi.
Nne, hawajengi ‘assets’. Watu wengi wakipata pesa wanafikiria kununua vitu. Lakini watu wanaojenga utajiri wanafikiria kununua assets.
Assets zinaweza kuwa biashara, hisa, ardhi, brand, ‘intellectual property’, ujuzi wa thamani na teknolojia. Assets ndizo zinazofanya pesa iiingie hata usipofanya kazi.
Tano, wanategemea chanzo kimoja cha kipato. Chanzo kimoja cha kipato ni hatari. Ukikosa kazi, biashara au mkataba, mapato yanaweza kusimama.
Watu wengi wanaofanikiwa huwa na vyanzo vingi vya kipato kupitia uwekezaji tofauti tofauti.
Sita, hawabadilishi ‘identity’ (utambulisho) yao. Hii ndiyo psychology ya ndani kabisa.
Kama mtu ndani yake bado anajiona maskini, asiyeweza au asiye na bahati, basi ataharibu hata fursa nzuri.
Akili yake itarudisha maisha kwenye kiwango alichozoea. Utajiri hauanzi kwenye akaunti ya benki. Unaanza kwenye fikra.
Somo kubwa. Pesa peke yake haiwezi kubadilisha maisha. Kinachobadilisha maisha ni ‘mindset’ (fikra), nidhamu, mfumo wa fedha na uwekezaji sahihi.
Mwisho, masikini wengi wakipata pesa hubadilisha maisha yao. Matajiri wakipata pesa hubadilisha assets zao. Ndiyo tofauti kubwa.
Mwalimu Benjamin Madaha ni mchambuzi mbobezi wa masuala ya fedha.
Makala hii imeandikwa na Benjamini Madaha


