5.7 C
New York

Mataifa yanayoongoza watu wake kwenda ughaibuni

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

NI kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa Idara ya Uchumi na Ustawi wa Jamii. Kwamba India inaongoza kwa raia wake kwenda nje ya nchi.

Kuondoka katika nchi yao kunaweza kuwa kunatokana na masomo, matibabu, kutafuta maisha, au sababu zingine.

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa raia wa China zaidi ya milioni 18 wako maeneo mbalimbali ulimwenguni.

China inashika nafasi ya pili ikiwa na watu wake milioni 11.7 wanaoishi nje ya Taifa lao hilo la barani Asia. Mexico inafuata katika nafasi ya tatu ikiwa na raia milioni 11.6.

Nchi zingine kwa mujibu wa UN ni Ukraine, ambayo ina watu milioni 9.8, Urusi (milioni 9.1), Syria (milioni 8.9), na Bangladesh (milioni 8.7).

Orodha hiyo inazijumuhisha pia Venezuela (milioni 8.3), Afghanistan (milioni 7.5), Ufilipino (6.9), Pakistan (6.9), na Misri (4.8).

Cha kushangaza, katika mataifa ya Guyana, Samoa na Bosnia, asilimia zaidi ya 50 ya raia wake wanaishi ughaibuni, moja ya sababu ikiwa ni kukimbia hali ngumu ya maisha.

Kwa nchi kama Sudan Kusini na Syria, sababu kubwa ya raia wake kukimbilia ‘ngambo’ ni kujinusuru na machafuko ya kisiasa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img