6.4 C
New York

Familia: Lungu hakulishwa sumu

Published:

LUSAKA, Zambia

FAMILIA ya Rais wa zamani wa Zambia, Edgar Lungu, imekanusha madai kuwa mwanasiasa huyo alikuwa kwa sumu.

Lungu hajazikwa tangu alipofariki Juni, 2025 akiwa kwenye matibabu nchini Afrika Kusini.

Polisi wa Afrika Kusini wanataka mwili wa kiongozi huyo ubaki kizuizini kwa ajili ya uchunguzi, kwa mujibu wa familia yake.

Hayo yanaibuka wakati bado hatima ya maziko haijafahamika kutokana na mvutano unaoendelea kati ya familia na Serikali ya Zambia juu ya anavyotakiwa kuzikwa.

Serikali, kwa upande wake, inataka Lungu azikwe kwa taratibu zao, wakati familia inashinikiza ishughulikie taratibu zote za kumpumzisha.

Lungu alifariki mjini Pretoria akiwa na umri wa miaka 68 na bado chanzo cha kifo chake hakijawekwa wazi.

Alikuwa Rais wa Zambia kuanzia mwaka 2015 hadi alipoondoka madarakani kwa kuzidiwa idadi ya kura na Hakainde Hichilema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2021.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img