CARACAS, Venezuela
MWANASIASA wa upinzani na mkosoaji mkubwa wa utawala wa Nicolas Maduro, Juan Pablo Guanipa, ameachiwa huru baada ya kushikiliwa na vyombo vya dola kwa miezi 10.
Ni mwezi mmoja sasa tangu utawala wa Rais Maduro ulipoondoshwa kwa kiongozi huyo kukamatwa na wanajeshi wa Marekani na kupelekwa mjini New York kwa ajili ya kusomewa mashitaka ya kujihusisha na utawala mbaya na biashara ya dawa za kulevya.
Kwa upande wake, Guanipa amerejea uraiani baada ya kuwa korokoroni tangu alipokamatwa Mei, 2025.
Kukamatwa kwake kulitokana na kauli ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Diosdado Cabello, ambaye alisema Guanipa anasuka mpango wa kuzuia Uchaguzi Mkuu.
Hatua ya Guanipa kuachiwa inakuja baada ya mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu, Maria Corina Machado, naye kurejea uraiani.
Machado, ambaye ni mshindi wa tuzo ya Amani’ ya Nobble, amesema bado wana jukumu kubwa la kuendeleza mapambano ya kuwakomboa raia wa Venezuela.
“Hatutopumzika hadi pale kila mfungwa wa kisiasa atakapoachiwa na kurudi nyumbani,” amesema Machado.


