10.7 C
New York

Utafiti: Idadi ya ‘wanaojichua’ imeongezeka Uingereza

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

IDADI ya watu ‘wanaojichua’ imeongezeka kwa kasi nchini Uingereza, huku wengi wao wakiwa ni wanaume, licha ya wanawake pia kujihusisha na vitendo hivyo.

Ni kwa mujibu wa utafiti mpya uliochapishwa katika Jarida maarufu la masuala ya ngono la Journal of Sex Research.

Matokeo ya utafiti huo yanaonesha kuwa kasi ya kujichua kwa makundi hayo imekuwa kubwa kuanzia mwaka 2000 hadi mwanzoni mwa miaka ya 2010.

Aidha, utafiti huo unaeleza kuwa chanzo kikubwa cha wanaume kujichua ni kukosa wenza wa kufanya nao mapenzi, ingawa wengine ni tabia hata wakiwa kwenye mahusiano.

Kwa wanawake, utafiti unadai kuwa wamekuwa wakijihusisha na vitendo hivyo pale wanapokabiliwa na changamoto ya kutokuridhishwa na wenza wao wanapokuwa faragha.

Utafiti uliohusisha watu 11,161 wenye umri kati ya miaka 16 na 44, ambapo idadi ya wanawake wanaojichua imeongezeka kwa asilimia 3.3, kutoka asilimia 37 hadi asilimia 40.3.

Kwa upande wa wanaume, ongezeko ni asilimia 4.1, yaani kutoka asilimia 73.4 hadi asilimia 77.5.

Wakati huo huo, rika la vijana wenye umri kati ya miaka 16 hadi 24 limeonekana kuwa wahanga wakubwa wa kujichua, kwa mujibu wa utafiti huo.

Ikumbukwe, kujichua kumekuwa kukihusishwa na matatizo mengi ya kiafya, ikiwamo kuathiri saikolojia, hivyo kusababisha kukosa kujiamini.

Pia, kitendo hicho kimekuwa kikitajwa kuathiri mishipa ya uume kwa kukiodhohofisha, hivyo kusababisha ugumba kwa mwanaume.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img