JAKARTA, Indonesia
WATU wawili wa jinsia tofauti wamecharazwa jumla ya viboko 140 kwa makosa makubwa mawili ya uzinzi na ulevi wa pombe.
Ifahamike kuwa vitendo hivyo ni kinyume cha sheria za Uislam (Sharia) zinazoliongoza Taifa hilo la barani Asia.
Mwanamke mwenye umri wa miaka 21 mkazi wa Jimbo la Aceh alipoteza fahamu baada ya kuzidiwa na idadi kubwa ya viboko alivyotandikwa na polisi watatu wa kike.
Katika tukio jingine, watu wanne, akiwamo ofisa wa polisi, nao walijikuta wakiangukia kwenye adhabu hiyo ya kutandikwa bakora kwa kosa la ulevi.
Kwa mujibu wa Sheria zinazotumika zaidi katika Jimbo la Aceh, uzinzi ni kosa na adhabu yake ni kutandikwa viboko 100, wati adhabu ya ulevi ni bakora 40.
Hata hivyo, adhabu hizo zimekuwa zikipingwa mara kwa mara na taasisi za kutetea haki za binadamu nchini Indonesia.
Azharul Husna, kiongozi wa Taasisi ya Haki za Binadamu ya Kontras, anasema adhabu hizo zimebeba sura ya udhalilishaji.


