10.5 C
New York

Marekani yajitoa WHO

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

SERIKALI ya Marekani imetangaza rasmi kujiondoa katika Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO).

Rais Donald Trump alisaini agizo la kujitoa WHO mwaka jana, hatua iliyokuja baada ya kulishutumu vikali Shirika hilo.

Katika shutuma zake, Trump akitambua kuwa Marekani imekuwa na msaada mkubwa kwa WHO, alisema Shirika hilo limekuwa likiipendelea China.

WHO imekanusha madai hayo ya Trump, pia ikisema kujitoa WHO si tu ni hasara kwa Marekani, bali pia kwa dunia kwa ujumla wake.

Kwa miaka mingi, Marekani imekuwa sehemu ya wafadhili wakubwa wa WHO lakini haijachangia kiasi chochote cha fedha tangu mwaka 2024.

Mbali ya kusitisha uchangiaji wa fedha, pia Marekani imewataka wataalamu wake ndani ya WHO kurejea nyumbani wakitokea Makao Makuu ya Shirika hilo mjini Geneva, Uswis.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img