LAGOS, Nigeria
POLISI wanamshikilia mtu mmoja, huku wakiendelea na uchunguzi juu ya kifo cha mwanamuzi wa Nigeria, Destiny Boy.
Destiny Boy, ambaye jina lake halisi ni Afeez Adesina, ni miongoni mwa wasanii chipukizi waliokuwa kwenye kiwango kizuri katika soko la Afrobeat.
Jina lake lilivuma kwa kasi mwaka 2019 baada ya kushirikiana na supastaa Davido katika wimbo maarufu wa ‘If’.
Taarifa za kifo chake zilitangazwa na familia Jumapili ya wiki iliyopita kwa kile ilichodai kuwa alikuwa na maradhi ya muda mrefu.
Hata hivyo, katika video zilizosambaa mitandaoni, mwili unaotajwa kuwa ni wakati wakati ukiingizwa mochwari umeibua maswali juu ya kifo chake.
Wengi wameonesha kutilia shaka juu ya chanzo cha kifo cha baba huyo wa mtoto mmoja, hivyo polisi nao wameamua kuingilia kati.


