9.5 C
New York

Messi agoma kuondoka Inter Miami

Published:

MIAMI, Marekani

SUPASTAA wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi, hana mpango wa kuondoka katika klabu ya Inter Miami ya Ligi Kuu nchini Marekani (MLS).

Taarifa hizo zinakuja wakati huu Messi akiwindwa na klabu tajiri ya Saudi Arabia, Al Ittihad, ambayo imeripotiwa kumtengea kitita cha Pauni bilioni 1.2.

Messi amekuwa mchezaji muhimu kwa Inter Miami tangu ilipmsajili mwaka 2023 akitokea Ulaya alikokuwa akiitumikia PSG ya Ligue 1.

Kwa miaka yake miwili akiwa na klabu hiyo ya Florida, nyota huyo amehusika katika mabao 121, licha ya kwamba amecheza mechi 88 pekee.

Akiwa na umri wa miaka 38 kwa sasa, ameigomea ofa ya Al Ittihad, ambayo ingemfanya kwenda kukutana na Cristiano Ronaldo anayekipiga Saudi Arabia akiwa na Al Nassr.

Ikumbukwe, alisaini mkataba mpya na Inter Miami mwishoni mwa mwaka jana, ambao utambakiza klabuni hapo hadi mwaka 2028.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img