8.4 C
New York

Nani kuvaa viatu vya Guardiola akiondoka City?

Published:

MANCHESTER, Uingereza

WIKI iliyopita, kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, alisema klabu hiyo inapaswa kujiandaa na maisha mapya bila uwepo wake kwenye benchi la ufundi.

Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 54, amekuwa kwenye benchi la timu hiyo kwa miaka tisa, akiipa mataji sita ya Ligi Kuu na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Guardiola amebakiza miezi 18 katika mkataba wake lakini kauli yake hiyo inaibua hofu kuwa huenda akaondoka Etihad kabla ya kuumaliza.

Kwa mujibu wa ripoti, tayari Mkurugenzi wa Michezo wa Man City, Hugo Viana, ameshaanza mchakato wa kusaka kocha atakayechukua nafasi ya Guardiola.

Eddie Howe

Hakuwa akipewa heshima kubwa katika soka la England lakini kwa sasa Howe anatajwa kuwa miongoni mwa makocha bora.

Howe anafanya vizuri Ligi Kuu ya England akiwa na Newcastle United, ambayo msimu uliopita aliipa ubingwa wa Kombe la Ligi (EFL Cup).

Enzo Maresca

Miongoni mwa wanaotajwa kwa sasa ni kocha huyo raia wa Italia, ambaye hivi karibuni alidai kuwa hapati sapoti ya kutosha kutoka kwa mabosi wa Chelsea. Maresca si mgeni pale Etihad kwani alikuwa sehemu ya wasaidizi wa Guardiola katika msimu wa 2022-23.

Unai Emery

Mhispania huyo anafanya kazi akiwa Aston Villa aliyoikuta ikiwa ‘timu ya kawaida’ na sasa inashiriki michuano ya Ulaya.

Kwa upande wa Ligi Kuu msimu huu, Villa imezidiwa pointi tatu pekee na Arsenal iliyojichimbia kileleni mwa msimamo.

Andoni Iraola

Ni kocha wa kiwango cha juu, akikumbukwa kwa namna alivyofanya Bournemouth kuwa timu tishio kwa vigogo msimu uliopita. Iraola aliiwezesha Bournemouth kumaliza msimu uliopita ikiwa nafasi ya tisa katika msimamo wa Ligi Kuu.

Oliver Glasner

Kocha wa kimatafa wa Austria. Kwa sasa, Grasner analiongoza benchi la ufundi la Crystal Palace.
Msimu uliopita ulikuwa mzuri kwa kocha huyo kwani aliiwezesha Palace kutwaa taji la FA ikiifunga Manchester City katika mchezo wa fainali.

Luis Enrique

Msimu uliopita, Mhispania huyo aliipa PSG mataji matatu, likiwamo la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo ya jijini Paris.

Endapo Enrique atakabidhiwa mikoba ya Guardiola, atakutana na kipa aliyemsugulisha benchi PSG, Gianluigi Donnarumma.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img