5.7 C
New York

Simulizi ya kusikitisha wafanyakazi wa ndani Lebanon

Published:

SHATILA, Lebanon

LEBANON imetajwa na watetezi wa haki za binadamu kuwa ni ‘jehanamu’ kwa baadhi ya raia wa kigeni wanaoingia nchini humo kwa lengo la kutafuta maisha kupitia kazi za ndani.

Taasisi za wanaharakati wa haki za binadamu zinaeleza kuwa nchi hiyo ina wafanyakazi wa ndani wa kigeni zaidi ya 150,000. Soma hapa

Abang Sharon ni msichana mwenye umri wa miaka 21. Aliondoka nchini kwao, Cameroon, na kuingia Lebanon mwanzoni mwa mwaka jana akiwa na ndoto za kupata ajira ili aweze kuisaidia familia aliyoaicha nyumbani.

Anasema ndani ya wiki mbili tu za mwanzo akiwa katika mazingira mapya nchini Lebabon, aliacha kazi katika nyumba mbili tofauti, hiyo ikitokana na mateso aliyokuwa akipata kutoka kwa mabosi zake.

Familia ya tatu ndiyo iliyokuwa hatari zaidi na kumpitisha katika safari ngumu zaidi kuwahi kuiona katika maisha yake.

“Nilianza kazi Mei, mwaka jana. Kama nilikotoka, sikuwa nikilipwa mshahara, sikuwa na mkataba wala huduma za msingi pale nilipohitaji.

“Wakati mwingine, bosi alitaka nikafanye usafi katika ofisi zake, licha ya kwamba nilikuwa mfanyakazi wa ndani,” anasema Sharon.

Licha ya kazi zote za ndani na zile za usafi ofisini, bado Sharon hakuwa akipewa mshahara wake wa Dola 200 kwa mwezi.

Mbaya zaidi, bosi hakuonesha kujali hata pale Sharon alipoanza kuumwa; akisumbuliwa na maumivu ya kifua na damu kutoka puani mara kwa mara. Alipokuwa anaumwa, alinyimwa chakula kwa madai kuwa hakuwa amefanya kazi.

Hata baada ya kupata msaada wa wanaharakati na kufanikiwa kurudi Cameron, Sharon aliambulia Dola 300 pekee kama malipo ya kipindi chote cha miezi nane ya kufanya kazi kwenye familia hiyo.

Mfumo wa unyonyaji

Sharon si msichana au mwanamke pekee anayepitia mateso hayo katika ajira hizo zisizo rasmi nchini Lebanon. Ni ajira zinazotumia mfumo maarufu uitwao ‘Kafala’ (ufadhili).

Katika mfumo huo, mwajiriwa kama Sharon anapokonywa hati ya kusafiria (passport) mara tu anapopatiwa ajira.

Hati hiyo anakuwa nayo mwajiri, hivyo ni ngumu kwa mwajiriwa kuondoka pasi na uamuzi wa bosi wake, hata pale anapozidiwa na mateso.

Kama hiyo haitoshi, wengi wao hawana vyumba vya kulala katika familia zilizowaajiri na badala yake huwekwa stoo au jikoni.

Melissa Kouame N’Guessan Epiphanie ni sehemu ya Taasisi ya Union Fait la Force (Pamoja Tunaweza) ya Lebabon, ambayo inajikita katika kutetea haki za wafanyakazi wa kigeni, hasa walio kwenye ajira sisizo rasmi kama Sharon.

Alianzisha Taasisi yake hiyo mwaka 2023 na kwa sasa inajivunia mafanikio makubwa, ikiwamo kuwa na wanachama 30 kutoka mataifa mbalimbali na kuwapatia makazi baadhi ya waganga.

Kwa kuwa naye alikuwa mfanyakazi wa ndani nchini Lebanon akitokea Ivory Coast, anafahamu vizuri mfumo huo wa ‘Kafala’.

“Mfumo wa Kafala una madhara makubwa. Wengi wanapokonywa hati za kusafiria, hawalipwi mishahara na wananyimwa uhuru,” anasema Melissa.

Taasisi nyingine inayojihusisha na utetezi wa haki za wafanyakazi wa aina hiyo ni Egna Legna Besidet, ambayo imejielekeza zaidi kwa wanawake kutoka Afrika, hasa Ethiopia.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img