5.7 C
New York

Mvua yaongeza majaga Gaza

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

WAKATI huu raia wengi wakiwa bado hawana makazi, mvua kubwa iliyonyesha kwa takribani wiki moja imesababisha hali kuwa mbaya zaidi.

Msemaji wa Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF), Jonathan Crickx, amesema kiwango kikubwa cha mvua kimeathiri maeneo mengi, ikiwamo jirani na ofisi yake.

Hofu kubwa ya Crickx ni kwamba watoto wako hatarini, kwani si tu wengi wao wanakosa makazi, bali pia sasa wanakabiliwa na janga la mvua kubwa katika kambi zao.

Katika mahojiano yake na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Crickx anatilia shaka kuwa huenda mvua hizo zikasababisha watoto kupata magonjwa.

Kwa upande wake, Wizara ya Afya ya Gaza inayoendeshwa na Kundi la Hamas imeripoti tukio la watoto 11 waliofarikia kwa kuangukiwa na jengo lililoangushwa na mvua.

Wakati huo huo, mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN) yameendelea na utaratibu wa kutoa misaada, ikiwamo mashuka na nguo kwa wakazi wa Gaza.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img