8.4 C
New York

Utafiti: Unapenda nyama? Soma hii…

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

LICHA ya kupendwa zaidi na wakati mwingine kuonekana ni kipimo cha ufahari, ulaji wa myama za kuku, nguruwe na ng’ombe huweza kubeba bakteria wanaosababisha maambukizi katika njia ya haja ndogo (UTI).

UTI ni ‘rafiki’ zaidi kwa wanawake, ambao tafiti zinaonesha kuwa ni asilimia 80, huku wengi wao wakiwa ni wenye umri wa kuanzia miaka 30. Dalili zake ni pamoja na maumivu wakati wa kujisaidia (haja ndogo), ambayo pia huenda ikaambatana na kwenda chooni mara kwa mara.

Sasa, utafiti uliochapishwa katika Jarida la mBio umebaini kuwa asilimia 18 ya maambukizi ya UTI hutokana na vyakula vitokanavyo na nyama.

Utafiti huo umeenda mbali zaidi na kutaja nyama za kuku, nguruwe na ng’ombe hubeba bakteria aina ya E.coli ambao husababisha UTI.

Akifafanua zaidi, Sherry Ross, ambaye ni Mtaalamu wa Afya ya Wanawake katika Kituo cha Afya cha St. Providence Saint John, anasema:

“Endapo nyama (ya kuku, nguruwe na ng’ombe) itakuwa imebeba E.coli, bakteria hao wanaweza kutembea (bila kuonekana) hadi mikononi (mwa mlaji).

“Ikiwa atashika sehemu za siri, ni rahisi kwa bakteria hao kuingia na kuufikia mfumo wa mkojo na kusababisha maambukizi.”

Utafiti ulihusisha wagonjwa wa UTI wapatao 23,483 kutoka majimbo nane ya California. Katika majibu, ilibainika kuwa walikuwa na bakteria 12,616 wa E.coli, ambao hupatikana kwenye nyama za kuku, nguruwe na ng’ombe.

Katika hatua nyingine, utafiti huo ulibaini kuwa kuku wanaongoza kusababisha UTI, wakifuatiwa na nguruwe, na kisha ng’ombe.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img