Na mwandishi wetu, Gazetini
RIPOTI ya mwaka huu ya mtandao wa OECD inaonesha kuwa Canada ndiyo kinara katika orodha ya nchi zenye wasomi wengi duniani, ambapo asilimia takribani 65 ya watu wazima wana elimu ya juu (chuo kikuu).
Kwa mujibu wa ripoti ya OECD, nchi zingine zinazofuata kwa watu wake wengi kuwa na Shahada (Degree) ni Jamhuri ya Ireland (57.5%) na Korea ya Kusini (56.2).
Mataifa mengine yanayoongoza kwa idadi kubwa ya wasomi ni Luxembourg (54.4%), Uingereza (53.8%), Australia (53.1%), Sweden (51.8%) na Marekani (50.7%).
Pia, kuna Israel (50.5%), Norway (50.4%), Lithuania (47.7%), Uswis (46.5%), Denmark (45.1%), Uholanzi (45.1%), Ubelgiji (45.0%), Iceland (44.5%), New Zealand (44.0%) na Ufaransa (43.4%).
Vilevile, kuna Finland (42.7%), Estonia (42.5%), Hispania (42.3%), Latvia (40.5%), Poland (39.5%), Austria (37.7%) na Ugiriki (35.3%).
Wakati huo huo, licha ya kiwango kidogo cha wahitimu wa elimu ya juu, mataifa ya Austria na Ujerumani yameelezwa kufanya vizuri kwa upande wa elimu ya ufundi.
Kwamba kwa kuwekeza zaidi katika ufundi, badala ya wingi wa wahitimu wenye vyeti, mataifa hayo yameonekana kufanya vizuri katika uuzalishaji wa ajira.
Mathalan, licha ya Ujerumani kuwa na asilimia 34 pekee ya watu wenye ‘Degree’, bado inafanya vizuri kiuchumi, ikishika nafasi ya 19 duniani kwa ukubwa wa Pato la Taifa.
Published:


