Na Mwandishi Wetu, Gazetini
JUMATANO ya wiki ijayo, Oktoba 29, Watanzania watapiga kura kuchagua rais, wabunge na madiwani. Ni haki ya Kikatiba inayotekelezwa kila baada ya miaka mitano.
Oktoba 29, Rais Dk. Samia atagombea kwa mara ya kwanza urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya miaka minne ya kushika nafasi hiyo kwa mujibu wa Katiba.
Katiba ambayo ilimtaka kuwa Rais akitokea katika nafasi ya Makamu wa Rais baada ya kifo cha John Pombe Magufuli mwaka 2021. Akawa mwanamke wa kwanza kukali kiti hicho katika historia ya soka la Tanzania.
Wakati raia wa Tanzania Bara wakiwa kwenye vituo vya kupiga kura, wenzao wa Visiwani Zanzibar nao watatekeleza haki hiyo Oktoba 29.
Zanzibar ina watu milioni 1.9, asilimia 98 wakiwa ni waumini wa Dini ya Uislam, na iliungana na Tanganyika mwaka 1964 na kuasisi Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lina wawakilishi 264, ambapo 214 ni kwa upande wa Bara na wengine 50 wanatokea Zanzibar. Vyama vya siasa 17 vinashiriki katika katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, huku Chama cha Mapinduzi (CCM) na ACT-Wazalendo (Alliance for Change and Transparency) vikiwa kwenye ushindani mkali baada ya CHADEMA kujitoa.
CCM imekuwa madarakani tangu ilipoasisiwa mwaka 1977 baada ya kuungana na Afro-Shirazi Party (ASP) cha Zanzibar. Kabla ya hapo, Tanzania ilikuwa chini ya TANU iliyoasisiwa mwaka 1954 na kukabidhiwa nchi baada ya uhuru mwaka 1961.
Mwaka 2015, CCM ilipata ushindani mkali kutoka kwa CHADEMA, ambapo mgombea urais wa Chama hicho cha upinzani, Edward Lowassa, alipata asilimia takribani asilimia 40 ya kura mbele ya Magufuli aliyeingia madarakani.
Mambo yalikuwa mabaya zaidi kwa upinzani katika Uchaguzi uliofuata, ambapo CHADEMA waliambulia asilimia 13 tu ya kura kwenye kiti cha urais.
Safari hii, CHADEMA hawatoshiriki Uchaguzi na sasa kiongozi wake wa juu, Tundu Lissu, ambaye pia ndiye aliyekuwa akitarajiwa kuwa mgombea wa urais, yuko gerezani kwa mashitaka ya uhaini.


